Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida ameondolewa kwenye hafla bila kujeruhiwa, baada ya mshukiwa kurusha kile kilichoonekana kuwa bomu la moshi kwenye hotuba yake nje ya eneo la Magharibi mwa Japan leo siku ya Jumamosi.
Vyombo vya habari vya ndani nchini humo vimeripoti picha na video zikionesha maafisa wakikabiliana na mshukiwa huyo huku umati wa watu ukikimbia kutoka katika eneo la tukio baada ya shambulio.
Korea kluwalipa milioni 1 kila mwezi vijana wanaosumbuliwa na upweke
Kishida alikuwa ameanza kutoa hotuba baada ya kuzuru bandari ya wavuvi huko Wakayama wakati kifaa hicho kiliporushwa na kujifunika kuashiria kujikinga.
Tukio hilo linawadia baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Shinzo Abe kuuawa kwa kupigwa risasi akiwa kwenye kampeni mwaka jana.