Waziri Mkuu: Tumeanza kuifanyia kazi ripoti ya CAG

0
38

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali tayari imeanza kuifanyia kazi taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) baada ya kuwasilishwa rasmi bungeni Aprili 6, mwaka huu.

Amesema hayo Aprili 13, 2023 wakati akihitimisha hoja zilizotolewa na Wabunge wakati wakijadili Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.

Mwanza: Magari yasimamishwa kwa saa nne ili Makamu wa Rais apite

Waziri Mkuu amesema anatambua hisia za wabunge pamoja na wananchi kwa ujumla kuhusu ubadhirifu wa mali na fedha za umma uliobainishwa kwenye taarifa hiyo, na kwamba miongoni mwa hatua zinazochukuliwa na Serikali ni kuhakikisha Maafisa Masuuli wote wanaandaa majibu ya hoja kama inavyoelekezwa katika sheria na kanuni za ukaguzi wa umma

“Nitumie fursa hii, kuwakumbusha Maafisa Masuuli wote wazingatie maelekezo ya Mheshimiwa Rais ya kuhakikisha wanapitia kwa kina taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kujibu na kuchukua hatua za haraka juu ya hoja zote zilizoibuliwa kwenye maeneo yao,” amesisitiza.

Ameongeza kuwa pamoja na hatua zinazochukuliwa na Serikali, taarifa ya kina kwenye maeneo yaliyobainishwa katika ripoti ya CAG, itawasilishwa bungeni kwa kuzingatia kanuni husika.

Send this to a friend