Waziri Mkuu: Tumemtoa TICTS tunamuweka DP World, hakuna geni

0
26

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekanusha madai ya watu wanaodai kampuni DP World imepewa bandari bila kikomo na kueleza kuwa kampuni hiyo itapewa kwa muda maalum kama utaratibu uliofanyika katika kampuni ya TICS.

Ameyasema hayo leo katika Alhamis Juni 29, 2023 wakati akihutubia Baraza la Eid El-Adh’haa lililofanyika katika Msikiti wa Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco mkoani Dar es Salaam.

“Hata huyu anayeondoka alianza kwa miaka 15 na baadaye akaongezwa miaka mitano na akoangezewa tena ikafika miaka 22, tukagundua ameshindwa kutekeleza majukumu kwa ufanisi. Tumesitisha mkataba, tunatafuta mwingine mzuri. Kwahiyo tunamuondoa TICTS tunamuweka DP hakuna jambo geni, hachukui bandari,” amesema.

Amesema wawekezaji wote walioko Tanzania hakuna aliyemilikishwa ardhi kwakuwa ardhi ya Tanzania ni ya Watanzania ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amekasimiwa kuisimamia, hivyo ikiwa kuna mwekezaji yeyote atajitokeza nchini atapewa kibali cha kufanya shughuli zake hapo.

“Kwahiyo na huyu akija tunampa kibali cha kukaa juu ya ardhi na akiwa hapo atalipa kodi ya kutumia ardhi,” ameeleza.

Waziri Mkuu amebainisha kuwa Serikali inaamini uwezo alionao DP World na wakati wa makubaliano Serikalini itazingatia maoni, ushauri na hofu ya Watanzania pamoja na kuwa makini ili taifa liweze kupata uchumi imara.

Send this to a friend