Waziri Mkuu: Tunazungumza na Denmark wasifunge ubalozi wao nchini

0
28

Serikali imesema kupitia Wizara ya Nje na viongozi wakuu, inafanya mazungumzo na nchi ya Denmark ili ofisi zao ziendelee kubaki nchini Tanzania kwa lengo la kuendeleza ushirikiano zaidi.

Ameyasema hayo leo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Chake Chake, Ramadhan Ramadhan aliyetaka ufafanuzi wa Serikali kuhusu baadhi ya balozi kutangaza kufunga ofisi zake nchini ikiwemo Denmark.

Waziri Mkuu amesema ni kweli Denmark imebadilisha sera za nchi na wanakusudia ifikapo mwaka 2024 kupunguza baadhi ya ofisi kwenye bara la Afrika ili kujikita kwenye nchi ambazo zina tatizo la kiusalama na hivyo Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye usalama.

Stika za TRA kwenye vinywaji: Wabunge walalamikia kampuni ya SICPA

“Tunataka tuone shughuli zetu zote ambazo ziko kwenye makubaliano yetu zinaendelea kama zilivyo na kwa kuwa mazungumzo yanaenedelea, tuna matumaini kwamba Denmark watatusikiliza Tanzania na wataendelea kubaki nchini. Na sisi tuendelee kushirikiano nao na tuendelee kunufaika na yale yote yanayoendelea kupatikana kupitia shirika lao linaitwa DANIDA,” amesema.

Ameongeza kuwa “Tanzania ina mahusiano mazuri na Denmark ya kidiplomasia, tumejikita kwenye siasa lakini pia kiuchumi, tunafanya biashara na tuna wawekezaji wako hapa nchini na Watanzania wachache waliowekeza Denmark wanaendelea na shughuli zao, na balozi wa Denmark alioko nchini Tanzania anaendelea kufanya kazi yake na hana matatizo,” ameeleza.

Send this to a friend