Waziri Mpango: Atakayevujisha siri za serikali atajutia ukaidi wake

0
49

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amelitaka baraza la wafanyakazi wizara hiyo kufanyakazi kwa kufuata misingi na kuwa hatasita kumchukulia hatua mtumishi atakayebainika kukiuka misingi na kutoa siri na taarifa nyeti za serikali.

Dkt. Mpango ameyabainisha wakati alipokuwa akifungua mkutano wa baraza kuu la wafanyakazi wa wizara hiyo amesema mtumishi yeyote atakayekiuka taratibu na miongozo hatavumilika.

“Natanguliza onyo kali kwa mtumishi yeyote atakayebainika kukiuka taratibu, miongozo na miiko ya kazi yake ndani ya Wizara ya Fedha na Mipango utajutia ukaidi wake,” amesema Dkt Mpango.

Aidha, amesema wafanyakazi hao kuwa wana majukumu makubwa katika mustakabali wa Taifa hasa wakati huu wa kutekeleza bajeti ya serikali katika majukumu yake.

Pia ametaka viongozi hao kuwa na utaratibu wa kuwasikiliza watumishi ili kupunguza au kuondoa malalamiko na manung’uniko ya wafanyakazi pindi wanapokuwa kazini ili wafanyekazi kwa utulivu kufikia malengo.

Send this to a friend