Waziri Mwakyembe ahoji sababu za Kocha Emmanuel Amunike kufukuzwa

0
40

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ametaka kuelezwa sababu za aliyekuwa Kocha Mkuu wa Tiu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Emmanuel Amunike kufukuzwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Waziri huyo mwenye dhamana aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumzia kukerwa na kitendo cha viongozi wa TFF kutohudhuria kikao alichoitisha jana, kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya soka nchini ikiwamo kuondolewa kwa kocha huyo.

Kikao hicho kilichoalika wadau mbalimbali kililenga kujadili sera ya wachezaji wa kigeni, kufukuzwa kwa kocha Emmanuel Amunike, na masuala mbalimbali ya maendeleo ya soka, lakini hakikufanyika kwa sababu TFF hawakuhudhuria, hivyo kikasogezwa mbele hadi Julai 24 mwaka huu.

Yapo mengi tuliyotaka tujadili, na kujua mikakati yao ijayo baada ya kumfukuza kocha ni ipi, kama wameiga Misri basi waige vizuri, alisema Waziri Mwakyembe.

Waziri Mwakyembe alifafanua kuwa sio kwamba anapingana na uamuzi wa kuondolewa kwa kocha huyo, lakini anataka kujua sababu za kuachana naye, nia mipango mikakati baada ya kuondoka kwa kocha, ambaye bado anadai mshahara wa miezi mitatu.

Aidha, Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao amesema walishindwa kuhudhuria kikao hicho kwa sababu walikuwa na matukio makubwa ofisini likiwemo la wakaguzi kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ambao wanafanya ukaguzi kwa siku mbili.

Wamesema kikao hicho awali kulipangwa kufanyika Julai 9, lakini kilihamishiwa Julai 10 kutokana na vifo vya wafanyakazi wa Azam Media Limited, na hivyo kuhamishwa huko kukaingiliana na ratiba nyingine, lakini walitoa udhuru.

Waziri alionya kuwa, endapo TFF hawatohudhuria kikao kijacho, watachukuliwa hatua.

Send this to a friend