Waziri Nape: Polisi ondoeni huruma kwa matapeli wa mtandaoni

0
14

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametangaza kiama kwa matapeli wote wa mitandao ya simu nchini ili Watanzania wabaki salama dhidi ya uhalifu huo.

Akizungumza leo bungeni jijini Dodoma amesema hapo mwanzo usajili wa laini za simu ulikuwa holela hivyo ilikuwa ni rahisi uhalifu kufanyika lakini Serikali ikaamua kuleta utaratibu wa usajili wa alama za vidole ambao pia uliruhusu uhalifu huo kufanyika, hivyo Serikali inaamini baada ya uhakiki laini zilizoko mtaani ni za wahusika.

“Tulichofanya tumezisajili laini zile kwa kutumia alama za vidole na penyewe ukawa na utapeli na ndo maana juzi tukafanya uhakiki, baada ya uhakiki tunaamini laini zote zilizoko mtaani zina mwenyewe na baada ya hapa nataka nitangaze kiama cha matapeli kwenye mitandao,” amesema.

Ukweli kuhusu mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo

Waziri Nape amesema Serikali imejipanga vizuri kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha utapeli kwenye mitandao unatokomezwa bila huruma yoyote.

“Nitaliomba bunge lako litusamehe kidogo, kwenye hili tutafunga macho kidogo hata kwenye zile haki za msingi kwa sababu yako mambo yanaudhi. Tumejipanga vizuri tutawaomba wenzetu wa polisi na wengine tuondoe huruma kwenye jambo hili tulikomeshe tulifute kwenye nchi yetu,” ameongeza

Send this to a friend