Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) unaendelea vizuri ambapo kipande cha kwanza na pili kutoka Dar es Salaam – Morogoro na Morogoro- Makutupora ujenzi umefikia asilimia 98 na asilimia 95, mtawalia, na majaribio ya uendeshaji yanatarajiwa kuanza mapema Desemba, 2023.
Amesema hayo Mjini Stockholm nchini Sweden alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Dhamana (EKN), Bi. Anna-Karin Jatko ambalo limetoa dhamana kwa mabenki mbalimbali yanayotoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa SGR.
Nissan kuuza magari ya umeme pekee ifikapo mwaka 2030
“Reli hii yenye urefu wa kilometa 2,102 ni muhimu kwa maendeleo na uchumi wa nchi na ni mradi wa kimkakati wa kikanda na ni kipaumbele cha nchi kwa hivi sasa kwa sababu utakuwa na matokeo makubwa kijamii na kiuchumi utakapokamilika,” amesema Dkt. Nchemba.
Dkt. Mwigulu amesema Serikali inakamilisha baadhi ya taratibu za mazingira na jamii kwa mujibu wa viwango vya kimataifa ili kukamilisha taratibu za upatikanaji wa rasilimali fedha kwa kipande cha tatu na nne.