Waziri Nchemba: Msiilaumu serikali bei kupanda, ni hali ya dunia

0
40

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali inaendelea kutafuta namna ya kukabiliana na ongezeko la gharama illiyosababishwa na janga la UVIKO19 pamoja na vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwigulu amesema miradi ya uchumi lazima iendelee licha ya kuwepo kwa majanga yanayoendelea duniani na kuongeza kuwa, Serikali inaandaa mkakati utakaosaidia unafuu wa bidhaa ikiwemo sukari, mafuta pamoja na usafirishaji.

“Sukari itakayoingia ambayo imekwisha agizwa tutapunguza kiwango cha kodi, kwa kiwango ambacho hakitakuwa chini ya asimilia 10 kwa muda mfupi huu wa sasahiv,.” amesema

Aidha, amegusia katika suala la kupanda kwa mafuta ya kula kwamba tayari wameelekeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waangalie hatua za muda mfupi ambazo wanaweza kuchukua, kisha wataelekeza viwango vipya vitakavyopunguza gharama.

Waziri amesema kuwa timu ya wataalamu watakaa kwa muda wa wiki moja waone ni hatua gani watakayochukua na waone wapi pa kugusa bila kuathiri sehemu yoyote.

Hata hivyo amewataka Watanzania kutokuilaumu Serikali kutokana na hali inayoendelea kwa kuwa ni jambo la dunia nzima, na kwamba Serikali ipo tayari kupokea maoni zaidi ili kuleta unafuu kwa wananchi

 

 

Send this to a friend