Waziri Nchemba: Serikali haina kesi za kodi za TZS trilioni 360

0
40

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali haina kesi 1,097 za kodi za muda mrefu zenye thamani ya shilingi trilioni 360 na dola za Marekani milioni 181.4 ambazo hazijaamuliwa.

Hayo yamesemwa bungeni leo Septemba 23, 2022 wakati akijibu swali la Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina aliyeuliza sababu zinazosababisha kesi 1,097 za kodi za muda mrefu zenye thamani iliyotajwa kutoamuriwa.

Waziri Nchemba amesema “Hadi Agosti 2022 kulikuwa na mashauri 854 kwenye hatua mbalimbali za usikilizaji , yenye kodi inayobishaniwa ya jumla ya shilingi trilioni 4.21 na dola za Marekani milioni 3.48 katika Bodi ya Rufaa za Kodi na Baraza la Rufaa za Kodi.”

Serikali yakaribisha maoni kuhusu tozo

Aidha, amesema kwa sasa taasisi za rufaa za kodi zinaendelea kusikiliza mashauri hayo pamoja na mashauri mapya yanayoendelea kusajiliwa.

Vilevile, amesema kwa nyakati tofauti idadi ya mashauri ya kodi hupungua au kuongezeka kulingana na kasi ya usikilizaji na usajili.

Send this to a friend