Waziri: Ndizi zilizokamatwa Zanzibar ziliingizwa kimagendo

0
36

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Mifugo na Biashara wa Zanzibar,  Shamata Shaame Khamis ametoa ufafanuzi juu ya tukio la mfanyabiashara, Veronica Mwanjala kutaifishwa tenga 30 za ndizi na kutozwa TZS 50,000 kwa madai kuwa Zanzibar haiitaji ndizi kutoka bara kwa kuwa inajitosheleza.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Waziri Shaame amepinga kauli hiyo na kueleza kuwa mzigo huo ulikamatwa kutokana  na taratibu ambazo imejiwekea Zanzibar kutoingiza ndizi kutoka nje kutokana na magonjwa yaliyoikumba migomba ya Tanzania Bara.

“Ni kweli tukio lipo lakini siyo kwa mazingira ambavyo linatangazwa kuwa Zanzibar inajitosheleza kwa ndizi ama kisa ni kutoka Tanzania Bara, uhitaji upo ila kwa mujibu wa sheria zilizopo haturuhusu kuingiza ndizi kwa sababu ya kuzuia ugonjwa ulioshambulia migomba,” amesema.

Waziri Mkuu: Msirekodi matukio na kuweka mitandaoni, pelekeeni mamlaka husika

Aidha, mbali na sababu hiyo ameeleza kuwa mwanamke huyo aliingiza mzigo huo kimagendo na hakuwa na kibali chochote huku akichanganya ndizo hizo na nyanya ili mzigo uonekane ni nyanya pekee, na kuhusu tenga akieleza kuwa hazikuwa tenga 30 bali 15.

Kuhusu kutaifishwa amedai walitoa pendekezo kwa mwanamke huyo kuzirejesha alipozitoa au kuziharibu mbele yake akishuhudia jambo ambalo amedai hakuonesha ushirikiano hivyo wizara imezihifadhi ndizi hizo.

Send this to a friend