Waziri Ndumbaro ajiuzulu TFF

0
54

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Damas Ndumbaro amejiuzulu uenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Leseni za Klabu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na wadhifa wake mpya.

Katika taarifa iliyotolewa na TFF imesema barua ya Waziri Ndumbaro kwa Rais wa TFF, Wallace Karia imebainisha kuwa kutokana na wadhifa wake wa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo inamlazimu kujiuzulu wadhifa huo ili kutekeleza majukumu yake mapya.

“Alisema amelazimika kujiuzulu nafasi hiyo ili atekeleze majukumu aliyopewa kwa haki na kuepusha mgongano wa maslahi,” imeeleza taarifa ya TFF.

Mchengerwa amsimamisha kazi Mkurugenzi halmashauri ya Busega

TFF imesema Rais Karia amepokea uamuzi huo na kumwahidi ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yake mapya.

Send this to a friend