Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa ametahadharisha wananchi kutofanya mauziano na manunuzi ya ardhi kwa fedha taslimu (cash) ili kuepuka utapeli.
Waziri Silaa ametoa tahadhari hiyo mkoani Tanga wakati wa ziara ya kufuatilia maelekezo ya Baraza la Mawaziri kuhusu migogoro ya vijiji 975 nchini, ambapo ameeleza kuwa amekuwa akikutana na malalamiko mengi ya wananchi yanayokuja kwake kama migogoro ya ardhi huku chanzo kikuu kikiwa ni mauziano yasiyo na ushahidi wa miamala.
Jalada la kesi ya Mbunge Gekul lamfikia DPP
“Biashara yoyote unayofanya na mtu akakung’ang’ania kumlipa pesa taslimu lazima kuna ulakini, kwa sababu anafahamu pesa taslimu haina ushahidi wa makabidhiano ya fedha, kwa hiyo ni vyema Watanzania wakajikita kwenye malipo ya kiutaratibu na ya kisheria. Unanunua ardhi kwa mtu akupe akaunti umtumbukizie fedha,” ameeleza.
Aidha, amesema Wizara ya Ardhi imejipanga kuboresha mifumo ya TEHAMA ili kuongeza kasi ya miamala ya ardhi, kuondoa usumbufu na kuchangia katika uchumi wa nchi.