Waziri Ummy asema Serikali inafuatilia tetesi za UVIKO19

0
46

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Wizara inachakata taarifa zilizokusanywa kutoka hospitali na vituo mbalimbali kisha itatoa taarifa endapo kuna ongezeko la magonjwa ya mfumo wa hewa au la.

“Kwa taarifa za wagonjwa waliopimwa virusi vya UVIKO-19 wiki tarehe 6 hadi12 Mei 2023, watu 6 kati ya 288 walithibitishwa kuwa na Korona.  Hii ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya Aprili 29, 2023 hadi Mei 5, 2023. Hakuna kifo chochote kilichosababishwa na UVIKO-19.,” amesema.

Waziri Ummy amewaomba wananchi kuendelea kuzingatia kanuni za afya ikiwa ni pamoja na kuzingatia usafi.

Send this to a friend