Waziri Ummy asitisha mfumo mpya ukusanyaji wa ada za maegesho ya magari

0
38

Serikali imesitisha kwa muda matumizi ya mfumo wa ukusanyaji wa ada za maegesho ya magari kwa kutumia mfumo wa kieleketroniki unaosimamiwa na Wakala wa Barbara za Vijijini na Mijini(TARURA) kuanzia leo Oktoba 9, 2021.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu akieleza kwamba amepokea malalamiko ya baadhi ya wananchi kuhusu changamoto zinazojitokeza wakati matumizi ya mfumo huo.

Amesema uamuzi huo ni muhimu licha ya dhamira nzuri waliyonayo TARURA katika kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa mapato yatokanayo na maegesho ya vyombo vya moto, matumizi ya hifadhi za barabara na tozo za adhabu zitokanazo na ukiukwaji wa matumizi ya hifadhi za barabara.

Sambasamba na hilo Waziri Ummy amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe kukutana na timu va Wataalamu wa TARURA kujadili namna ya kutatua changamoto zilizojitokeza, wakati huo huo, ukusanyaji wa ada za maegesho ya magari ukiendelea kukusanywa kwa kutumia mfumo wa awali(Manual system) ambao ulikuwa unatumika kukusanyia ada hiyo kabla ya kuanza kutumia mfumo wa kielektroniki
(TeRMIS).

Mfumo wa Kieleketroniki wa ukusanyaji wa ada za maegesho ulianza kutumika katika mkoa hivi karibuni lengo ikiwa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa chanzo hicho na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali.

Send this to a friend