Waziri Ummy atoa tamko kuhusu mtumishi aliyeosha vifaa vya hospitali kwa maji baridi

0
33

Kufuatia kipande cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii kikimuonesha mtumishi wa afya katika hospitali ya Kivule akisafisha vifaa vya hospitali hiyo kwa maji baridi, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanalifanyia kazi na watatoa taarifa rasmi kuhusu suala hilo.

“Nimeona clip inayohusu mtumishi wa afya akichambua, kusafisha na kuanika vifaa vya hospitali katika Hospitali ya Kivule mkoani Dar es Salaam. Kitendo hiki ni kinyume na taratibu na miongozo ya Kanuni za Udhibiti wa Maambukizi (Infection Prevention and Control). Tayari Viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam wanalifanyia kazi suala hili na watatoa taarifa rasmi.

Waziri Masauni amuonya Zumaridi, asema kanisa lake halijasajiliwa

Ninamshukuru mwananchi aliyerekodi na kuisambaza clip hii. Nitoe wito kwa wananchi kutoacha kuibua mambo kama haya yanayotokea katika vituo vyetu vya kutoa huduma za afya vya umma na binafsi ili kuongeza uwajibikaji katika utoaji wa huduma za afya nchini kwa kuwa afya zetu ni wajibu wetu,” amesema.

Aidha, Waziri Ummy ametoa rai kwa wataalamu wa afya kuzingatia mafunzo na miiko ya kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuongeza kuwa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na ofisi ya TAMISEMI zitaendelea kuchukua hatua ili kuimarisha ubora wa huduma.

Send this to a friend