Waziri wa Uganda auawa na mlinzi wake

0
41

Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano ya Viwanda nchini Uganda, Kanali Mstaafu Charles Okello Engola ameuawa kwa kupigwa risasi asubuhi ya leo na mlinzi wake kutoka nyumbani kwake.

Spika wa Bunge nchini humo, Anita Among amethibitisha kifo cha waziri huyo alipokuwa akiongoza kikao cha mashauriano leo asubuhi.

“Leo asubuhi, nilipata taarifa za kusikitisha kuwa Mheshimiwa Engola amepigwa risasi na mlinzi wake. Roho yake ipumzike kwa amani. Huo ulikuwa mpango wa Mungu, hatuwezi kubadilisha chochote,” amesema Among

Watoto 900, wajawazito 57 wafariki kwa kukosa huduma za uzazi

Mshambulizi huyo ambaye bado hajafahamika hadharani anaripotiwa kujipiga risasi kwa mujibu wa shirika la utangazaji la serikali UBC.

Bado haijulikani chanzo cha tukio hilo na kwa sasa maafisa wa usalama wamezingira eneo hilo la tukio kwa uchunguzi zaidi.

Send this to a friend