Wezi wachomwa moto kwa kuiba michango ya mazishi

0
48

Washukiwa wawili kati ya tisa wa genge la uhalifu wameuawa na miili yao kuchomwa moto baada ya kuvamia katika hafla ya kuchangisha pesa za mazishi huko Mombasa.

Ripoti zinasema kuwa wawili hao waliochomwa moto kiasi cha kutotambulika, walikuwa miongoni mwa washambuliaji tisa waliokuwa na silaha yakiwemo mapanga ambao walivamia tukio hilo kabla ya kuwashambulia na kuwaibia waombolezaji waliokuwepo.

Madagascar yapitisha sheria ya kuwahasi wabakaji wa watoto

Ripoti ya polisi imeeleza kuwa wezi hao waliiba kompyuta ndogo, vyombo vya muziki, simu na pesa taslimu pamoja na kuharibu magari matatu.

Hata hivyo, kufuatia tukio hilo, kundi la watu liliamua kuwasaka washukiwa hao na kuwachoma moto, na kisha miili hiyo kuhifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi.

Send this to a friend