WhatsApp kuwezesha watumiaji kuhariri (edit) ujumbe

0
50

Baada ya Mtandao wa WhatsApp kutangaza kuongeza kipengele cha kuondoka kwenye kikundi bila ya kuonesha taarifa kwa wana kikundi, inadaiwa kuwa mtandao huo uko mbioni kuongeza kipengele kingine cha kusahihisha (edit) ujumbe uliotumwa.

Kulingana na WABetaInfo (kupitia 9to5Mac), imeeleza kuwa mtandao wa WhatsApp tayari unatengeneza kipengele hicho ambacho kitaruhusu mtumiaji kurekebisha ujumbe uliotumwa na kuutuma tena.

Haijulikani ikiwa ujumbe utaweza kuhaririwa muda wowote au ndani ya dirisha la muda fulani.

WABetaInfo inadai kuwa kipengele hiki bado hakipatikani kwa wanaojaribu kutumia ‘beta’, lakini pengine kitaonekana hivi karibuni, inapaswa pia kupatikana kwenye WhatsApp kwa iOS.

WhatsApp iliongeza uwezo wa kufuta ujumbe uliotumwa miaka mitano iliyopita na pia hivi majuzi imeongeza vipengele kadhaa vinavyohitajika, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuchapisha majibu ya ujumbe pamoja na kuunda vikundi vinavyokaribisha hadi watu 512.

Send this to a friend