WhatsApp yabadili masharti ya kujitoa kwenye kikundi

0
18

Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa WhatsApp, kwa sasa wataweza kujitoa kwenye makundi waliyounganishwa kwa siri.

Kutokana na ripoti ya WABetaInfo iliyotolewa Mei 18, watu binafsi wataruhusiwa kuondoka kwenye vikundi bila ya kuwepo na kidokezo cha kuwataarifu wanachama kuhusu kuondoka kwao.

Jarida hilo pia lilionesha kuwa kipengele hicho ambacho bado kilikuwa tayari kinaundwa lakini hakikutoa habari kuhusu ni lini kitaanza kutekelezwa kote ulimwenguni.

Maendeleo hayo yakikamilika yataondoa kipengele cha sasa ambacho kinawajulisha wanachama wote pindi mmoja wao anapoamua kuondoka au kuondolewa na wasimamizi wa kikundi.

Katika kipengele kipya, mtu anapochagua kuondoka kwenye kikundi, ni wewe tu na wasimamizi wa kukundi mtajulishwa kuwa umeondoka kwenye kikundi.

Hata hivyo, bado haijulikani ikiwa washiriki wote watajulishwa wakati msimamizi mmoja atamwondoa mtumiaji kutoka kwa kikundi fulani.

Send this to a friend