WHO: Idadi ya vifo Uturuki na Syria yaweza kufikia 20,000

0
51

Idadi ya watu walioripotiwa kufariki nchini Uturuki na Syria inakaribia watu 5,000, na watu 15,000 wakijeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Jumatatu.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) idadi ya vifo nchini Uturuki na Syria inaweza kufikia 20,000 hivi karibuni kwa sababu ya mamia ya watu ambao bado wamefunikwa na vifusi .

Waokoaji wanapambana na mvua kubwa na theluji kutafuta manusura wa tetemeko hilo huku ikiripotiwa kuwa takribani meli 10 na ndege ndogo 54 zikitumika kusafirisha majeruhi na kusaidia katika shughuli za utafutaji.

 Aidha, tetemeko la kipimo cha magnitudi 5.4 limeripotiwa kusikika mashariki mwa Uturuki asubuhi ya leo hali inayowapa hofu wakazi wa eneo hilo kurudi majumbani mwao.

Send this to a friend