WHO kufanya majaribio ya Chanjo ya Ebola nchini Uganda

0
34

Kutokana na kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda, Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema liko mbioni kuanza majaribio ya chanjo moja au mbili dhidi ya aina ya virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini humo.

Bodi ya Afya ya WHO imesema inasubiri idhini kutoka Serikali ya Uganda, na kwamba endapo itaidhinishwa zoezi hilo la chanjo linaweza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Oktoba au mapema mwezi ujao.

Tanzania na Kenya kuondoa vikwazo vya kibiashara vilivyobaki

Taarifa iliyotolewa hivi karibuni kutoka Wizara ya Afya ya nchi hiyo imesema hadi wakati huo wagonjwa 43 wamegundulikana kupata maambukizi hayo huku wagonjwa 10 wakifariki kutokana na maambukizi hayo.