WHO: Watanzania wengi wanaokwenda nje ya nchi wana COVID19

0
30

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameitaka Tanzania kutumia njia zinazoaminika kuwa zinazuia maambukizi ya virusi vya corona, itoe takwimu kuhusu visa vya ugonjwa huo na ijiandae kupokea chanjo.

Dkt. Tedros Ghebreyesus ametoa wito huo kupitia taarifa yake kwa Tanzania kuhusi ugonjwa aa COVID19 ambapo amesema kuwa amewasiliana na viongozi mbalimbali wa Tanzania lakini hajapokea mrejesho wa mkakati wa Tanzania kukabiliana na virusi hivyo.

Amesema idadi kubwa ya Watanzania wanaokwenda nchi za jirani wanakutwa na maambukizi ya #COVID19 na kwamba hilo linatia chachu kwa Tanzania kuchukua tahadhari kulinda raia wake, raia wa nchi jirani na kwingineko.

“COVID19 ni ugonjwa hatari unaweza kusababisha mtu kuumwa sana na hata kifo. Mataifa yote yanapaswa kufanya kila wawezalo kulinda watu na kuokoa maisha na WHO iko tayari kushirikiana nayo kukabiliana na virusi hivi hatari,” imeeleza taarifa ya Ghebreyesus.

Katika hatua nyingine ametoa pole kwa Tanzania kwa kuondokewa na wanasiasa nguli pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi hivi karibuni.

Send this to a friend