Wimbo wa Harmonize wafutwa mitandaoni

0
36

Uongozi wa Konde Music Worldwide ya manamuziki Harmonize umeomba radhi kutokana na maudhui ya wimbo uliotolewa hivi karibuni na msanii huyo unaoitwa ‘Weed Language’ kwenda kinyume na sheria na tamaduni za nchi.

Lebo hiyo imedai kuwa lengo la kutoa wimbo huo lilikuwa kupanua na kukuza muziki wa nje ya mipaka ya nchi ya Tanzania.

Taarifa hiyo imetolewa leo katika ukurasa wa Instagram ya msanii huyo baada ya kuonekana katika picha akiwa na viongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) hapo jana Desemba 7, 2022 huku akiahidi kutekeleza suala walilozungumza kama vijana.

Aslay ataja kilichosababisha apotee kwenye muziki

Katika taarifa iliyotolewa leo imesema “kutokana na kadhia iliyosababishwa na maudhui ya wimbo huo, tunaomba radhi na tunaahidi kuuondoa wimbo huo kwenye mitandao yote ya kijamii.”

Jana Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Gerald Kusaya alitoa onyo kwa wasanii wa Tanzania wanaotunga nyimbo za kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi na kusema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wasanii hao.

Send this to a friend