Wizara ya Afya: Gharama ya kupima COVID-19 nchini ni TZS 231,000

0
14

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imetoa toleo jipya la muongozo upimaji maambukizi ya viusi vya corona (COVID19) kwa wanaosafiri kwenda nje ya nchi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanaoambukizwa virusi hivyo duniani na kuwepo kwa vimelea vipya katika baadhi ya nchi.

Muongozo huo umeweka utaratibu wa maombi, upimaji, upataji wa majibu ya vipimo, uhakiki mipakani na gharama za kupima.

Muongozo umeelekeza kuwa gharama ya vipimo ni $100 (TZS 231,900) na kuwa majibu ya vipimo yatatolewa ndani ya saa 24 kwa mkoa wa Dar es Salaam na ndani ya saa 48 kwa mikoa mingine.

Katika muongozo uliotolewa Julai 2020, gharama za vipimo vya COVID-19 zilikuwa kama ifuatavyo kwa kila safari;
• Raia wa Tanzania: Tsh.40,000/=
• Raia Mkaazi wa Tanzania: Tsh.60,000/=
• Raia wa Kigeni: USD.100

Send this to a friend