Wizara ya Afya: Waziri Mkuu hajadanganya kuhusu wimbi la nne la UVIKO19

0
39

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kwamba taarifa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwamba hakuna wimbi la nne la UVIKO19 na ile ya Katibu Mkuu Afya, Prof. Abel Makubi kuhusu kuongezeka kwa maambukizi ya UVIKO19, zote ni sahihi.

Prof. Makubi amesema kwamba taarifa hizo hazikinzani kabisa kwani kuongezeka kwa maambukizi au visa hakumaanishi kuwa tayari ni wimbi jipya la maambukizi.

“Sisi hatuna mgonjwa hata mmoja wa wimbi la nne [Omicron]. Yote hiyo ni vita ya kibiashara, kwa hiyo sekta binafsi mtusaidie kusema haya, tukiacha watu wakapotosha wataharibu nchi,” alisema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Desemba 11 mwaka huu.

“Wimbi ni tofauti, na ongezeko linatokea ghafla au kwa kipindi kifupi. Ili kusema kuna wimbi jipya ni lazima hali ya ongezeko iendelee kwa kipindi fulani (walau kati ya siku 14-21),” ameeleza Prof. Makubi kwenye taarifa yake kwa umma.

Amewataka wananchi kupuuza upotoshaji wa taarifa sahihi za viongozi wote wawili na zimetolewa kwa wakati tofauti kama mwendelezo wa serikali kuwasiliana na umma.

Aidha, wananchi wamehimizwa kuendelea kuchukua tahadhari kujikinga na UVIKO19, kwani ugonjwa huo bado upo na maambukizi yamekuwa yakiongezeka.

Send this to a friend