Wizara ya Afya yawataka wananchi kuvaa barakoa inapolazimika

0
28

Wizara ya Afya imewataka wananchi kuendelea kuchukua tahahdari dhidi ya COVID19 ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa pale inapolazimika, kutokuwa na hofu zinazojengwa na upotoshaji na kuendelea kunawa mikono mara kwa mara.

Taarifa ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi imeeleza kuwa kutokana na namna ugonjwa huo unavyoendelea katika mataifa mengine, ni vyema wanachi wakaendelea kuchukua tahadhari.

Aidha, Prof. Makubi amewasihi wananchi kuendelea kufanya mazoezi mara kwa mara, kula lishe bora, kutambua hali za afya zao ili waweze kujilinda pamoja na kuendelea kutumia tiba asili.

Wizara imewataka wananchi pia kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza ikiwa ni pamoja na kupunguza ulaji wa mafuta, chumvi nyingi, unywaji pombe na uvutaji wa sigari.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, magonjwa yasiyoambukiza yanachangia takribani asilimia 40 hadi 45 za vifo hospitalini ikiwa ni ongezeko kutoka asilimia 33 kwa miaka mitano iliyopita.

Send this to a friend