Wizara ya Maliasili imepania kuendeleza hali bora ya wafanyakazi wakati huu sekta hizo zikiendelea kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa nchi ikiwemo kuongoza kwa kuingiza fedha za kigeni kwa asilimia 25.
Waziri wa Utalii, Angellah Kairuki amesema hayo wakati akifungua Kikao cha 31 cha Baraza la Wafanyakazi ambapo pia amewepongeza wafanyakazi wa wizara hiyo na taasisi zake kwa utendaji na kufikia mafanikio mengi na kutaka wajitume zaidi hasa kuhifadhi na kuongeza zaidi idadi ya watalii nchini.
Awali, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi na Mwenyekiti wa Baraza hilo alieleza mafanikio ya kiutendaji ikiwemo wizara hiyo kuwa ya kwanza kuhamia jengo jipya mji wa Serikali Dodoma, kununua magari mapya na vitendea kazi vingine na kuishukuru Serikali kwa kuongeza bajeti ya wizara hiyo katika mwaka ujao wa fedha.