Wizara ya Mambo ya Nje yafafanua kuondolewa Balozi wa Tanzania nchini Kenya
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imekanusha taarifa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Pindi Chana ameondolewa kwenye wadhifa wake kutokana na mgogoro wa mipaka kati ya Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Kanali Wilbert Ibuge amesema kuwa muda wa balozi hiyo ulimalizika Disemba 2019, na kwamba kuchelewa kuteuliwa kwa mrithi wake ni saula la kawaida la kidiplomasia.
Ibunge ametoa taarifa huyo kufuatia baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kuwa Dkt. John Simbachawene ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, akichukua nafasi Dkt. Chana, ambaye ameondolewa kutokana na mgogoro wa mipaka baina ya nchi hizo mbili.
Dkt. Simbachawene aliapishwa Mei 21 mwaka huu pamoja na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania kwenye nchi za Algeria na Msumbiji.