Wizara ya Mambo ya Nje yasema haina taarifa za vikwazo vya Marekani

0
13

Siku mbili baada ya Marekani kutangaza kuwawekea vikwazo baadhi ya maafisa wa Tanzania kwa kuvuruga uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema haina taarifa hiyo.

Msemaji wa wizara hiyo, Emmanuel Buhohela amesema kuwa wameona jambo hilo mitandaoni na kwamba hawafanyii kazi taarifa za kwenye mitandao.

“Hatujapata taarifa rasmi zaidi ya kuona katika mitandao na hatuwezi kufanyia kazi vitu vya mitandaoni. Wizara yetu ina utaratibu mzuri wa mawasiliano na Balozi na hatujaletewa taarifa rasmi,” amesema Buhohela.

Wakati wizara ikisema hayo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) zimesema kuwa kunapokuwa na malalamiko ya kuingilia uchaguzi, sheria zipo za kufuata kushughulikia hilo.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage amesema Marekani ieleze uchaguzi huo uliingiliwaje kwa sababu kulikuwa na waangalizi makini na ripoti zao zinaeleza wazi mchakato mzima wa uchaguzi ulivyofanyika.

Januari 19, 2021 aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo alitoa taarifa kuwa baadhi ya maafisa wa Tanzania wamewekewa vikwazo vya kusafiri kutokana na kuvuruga mchakato wa kidemokrasia wakati wa uchaguzi.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijawata watu walioelezwa kuwekewa vikwazo.

Send this to a friend