Wizara ya Mambo ya Nje yatangaza nafasi za ajira

0
43

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imetangaza nafasi za muda za ajira katika Jumuiya ya Madola kwa watanzania wenye sifa.

Wizara imetangaza nafasi hizo kuwa ni za mkataba wa miaka miwili katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola chini ya Mpango wa Wataalamu wa Vijana (YPP).

Tangazo la nafasi ya kazi Mfuko wa Utamaduni na Sanaa

Maelezo zaidi kuhusu vigezo na taratibu za utumaji wa maombi yanapatikana kupitia tovuti ya http://thecommonwealth.org/jobs.

Mwombaji anapaswa kuwa na umri usiozidi miaka 27, na mwisho wa kutuma maombi hayo ni Agosti 8, 2022.

Send this to a friend