Wizara yapendekeza mikutano na upigaji kura vifanyike kwa mtandao

0
39

Wizara ya Fedha na Mipango- Zanzibar imependekeza matumizi ya teknolojia ya kisasa katika michakato ya uchaguzi ili kupunguza changamoto zinazojitokeza ikiwemo uwazi wa kupiga kura, utangazaji wa matokeo na gharama za kuagiza karatasi za kupigia kura kutoka nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu- TEHAMA, Rashid Rashid alipowasilisha maoni mbele ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

Rashid amesema mfumo huo utasaidia vyama vya siasa kuacha kutumia mawakala katika vituo vya kupigia kura pamoja na kuondoa malalamiko na wasiwasi juu ya utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

MUHAS yagundua dawa za kuongeza kumbukumbu

“Mfumo huu utahusisha hadi kupiga kura kwa mfumo huo wa kielektroniki na tunataka uanzie huko tangu mtu anapiga kura mpaka matokeo yanatoka, mifumo yote iwe kidigitali na hiyo itapunguza gharama za kuendesha uchaguzi” amesema.

Aidha, amesema kuhusu elimu ya uraia, Wizara imependekeza Serikali na vyama vya siasa kuona haja ya uendeshaji mikutano yao kwa njia ya kidigitali ili kusaidia kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.

“Tunaona Rais wetu Zanzibar anafanya vikao kila mwezi, anafanya na Watanzania wanaoishi nje, Diaspora na wengi wanahudhuria, hili linawezekana, na katika kutekeleza, ni lazima elimu itolewe kwa mfumo huo,”ameongeza.

Send this to a friend