Yafahamu maswali 12 utakayoulizwa wakati wa sensa ya watu na makazi

0
33

Ofisi ya Taifa ya Takwimui (NBS) inaendelea na maandalizi ya Sensa ya watu na makazi ya itakayofanyika Agosti mwaka 2022 nchini Tanzania.

Sensa hiyo inatarajiwa kuwa tofauti na zilizopita kwani itahusisha masuala tofauti ikiwemo matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika ukusanyaji wa taarifa, lakini pia itakusanya taarifa za makazi.

Ili kufanikisha hilo, watu wote wanaokuwepo nchini siku ya sensa wataulizwa maswali 12 ambayo ni;

  1. Taarifa za kidemografia (umri, jinsi, uhusiano, hali ya ndoa, uraia, n.k.);

2. Maswali yanayohusu ulemavu;

3. Taarifa za Elimu;

4. Maswali ya uhamaji, pamoja na taarifa za Watanzania wanaoishi nje ya nchi

5. Maswali kuhusu umiliki wa nyaraka za kitaifa (vitambulisho vya NIDA, Mzanzibari mkazi, cheti cha kuzaliwa, hati ya kusafiria, na leseni ya udereva)

6. Shughuli za kiuchumi

7. Umiliki wa ardhi na taarifa za TEHAMA

8. Taarifa za Uzazi na Vifo vilivyotokea ndani ya kaya

9. Vifo vitokanavyo na uzazi

10. Hali ya nyumba za kuishi na umiliki wa rasilimali mbalimbali

11. Maswali ya kilimo na mifugo

12. Mifuko ya hifadhi ya jamii.

Sensa ya mwaka 2022 itakuwa ni sensa ya sita kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.

Send this to a friend