Yakubu: Uwanja wa Benjamini Mkapa unatumika sana

0
35

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Said Yakubu amesema miongoni mwa vitu walivyoshauriwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) baada ya ukaguzi wa Uwanja wa Benjamin Mkapa ni pamoja na kupunguza matumizi ya uwanja huo.

Akizungumza katika kipindi cha Jambo Wikiendi cha TBC Machi 18, 2023 Katibu Mkuu amesema katika viwango vya kimataifa, uwanja unatakiwa usitumike zaidi ya mara mbili kwa wiki, lakini Uwanja wa Benjamin Mkapa umekuwa ukitumika katika mechi mbalimbali ikiwemo mechi za Simba na Yanga, matamasha pamoja na matukio mengine.

Ameongeza kuwa Serikali ina mpango wa kuufunga uwanja huo Machi 28, mwaka huu mara baada tu ya mechi ya Taifa Stars na Uganda ili kufanya marekebisho mbalimbali ikiwemo ukarabati mkubwa, lakini pia ukarabati mdogo ambao tayari umeanza kufanywa na wakandarasi wa ndani.

Hata hivyo, amesema uamuzii huo utazingatia endapo Simba na Yanga zitafanikiwa kufuzu hatua za robo fainali za mashindano ya CAF.

Eng. Hersi: Feisal bado hajarudi kambini, anadanganywa

“Ntakupa mfano mdogo tu, pale uwanjani Screen ambayo tunayo pale ina miaka 17, nadhani hata nyumbani kwako sidhani kama TV unakaa nayo miaka 17, baada ya muda ile TV itataoka, ni kwa sababu muda wake hauendani na wakati wa sasa,” ameeleza Katibu Mkuu.

Sababu kubwa zinazopelekea ukaguzi wa CAF uliofanyika katika uwanja huo ni kutokana na klabu ya Simba kuwa miongoni mwa nchi nane za Afrika zitakazocheza Africa Super League ambapo klabu zote zimetembelewa kwa ajili ya kukaguliwa vifaa vyao, viwanja vilivyochaguliwa kutumika na kuwasiliana kuhusu taarifa za ushiriki wao.

Send this to a friend