Yanayosemwa baada ya Rais kumteua Simbachawene aliyejiuzulu uwaziri 2017

0
35

Rais Dkt John Pombe Magufuli amemteua George Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira uteuzi ambao unaanza leo Julai 21, 2019.

Simbachawene ameteuliwa kushika nafasi hiyo kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi wa January Yusuf Makamba, mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga.

Uteuzi huo umeibua mijadala mitandaoni ambao wengi wanaohoji uamuzi wa Rais kumrejesha katika baraza la mawaziri, Simbachawene ambaye alijiuzulu mwaka 2017 kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili.

George Simbachawene alijizulu nafasi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) baada ya jina lake kuonekana katika ripoti zilizotolewa na kamati ya bunge katika uchunguzi kuhusu madini ya Tanzanite.

Kamati ya Bunge iliyoundwa kuchunguza sakata hili ilitaka Simbachawene aulizwe ni kwa nini alitoa uhamisho wa hisa za Sky Associate bila kuhusisha wataalamu, kwa sababu kamati ilishindwa kuelewa ni kwa nini alifanya hivyo.


Kwa muktadha huo, ridhaa iliyotolewa Januari 30, mwaka 2015 na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo, George Simbachawene, ina dosari za kisheria na ukiukwaji wa kiutendaji na utoaji wa ridhaa hii, unainyima STAMICO kipaumbele cha kununua Kampuni ya TML.

Kamati ilieleza kuwa waziri aliamua kutoa ridhaa bila ya kuzingatia ushauri wa mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini na katika hilo, kuna barua ya ushauri wa mwanasheria iliyosema uuzwaji wa hisa hizo sio halali kwa sababu mtu huyo hatumfahamu.

Kufuatia mambo hayo, Septemba 7, 2017 Simbachawene alijiuzulu nafasi yake.

Wengi wanaohoji wanatumia ahadi ambayo Rais Dk Magufuli amekuwa akiyasema mara kwa mara kwamba mtu akishaharibu sehemu moja, aondolewe na sio kupelekwa sehemu nyingine ili akaharibu tena.

Wakosoaji hao wanahoji kama tukuma zinazomkabili Simbachawene hazipo tena, au kwanini Rais ameamua kumrudisha serikalini wakati alijiuzulu mwenyewe kutokana na tuhuma hizo.

Hapa chini ni baadhi ya waliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter kuhusu uteuzi huo:

Baada ya utenguzi huo, Mbunge January Makamba amesema kuwa amepokea kwa moyo mweupo mabadiliko hayo, na kwamba atazungumza mbeleni.

https://twitter.com/JMakamba/status/1152798935355985922
Send this to a friend