Yanga: Mchango wa milioni 100 ulitoka GSM Foundation

0
129

Klabu ya Yanga imesema mchango wa TZS milioni 100 uliotolewa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ulitolewa na taasisi ya GSM chini ya mdhamini na mfadhili wa klabu, Ghalib Mohamed na sio kupitia pesa za wanachama au kutoka kwenye mfuko wa klabu.

Kauli hiyo imekuja kufuatia malalamiko mengi kutoka kwa wanachama na mashabiki wa klabu hiyo, wengine wakidai pesa hizo ambazo Yanga ilichangia kwa ajili ya kampeni ya uchaguzi mkuu wa CCM, pengine zimetolewa kutoka mfuko wa klabu hiyo.

“GSM Foundation imekuwa ikishirikiana na Klabu ya Yanga kwa kipindi cha miaka mitatu kutoa fedha na misaada kwa jamii na makundi mbalimbali ndani na nje ya mipaka ya Tanzania,” imeeleza taarifa iliyotolewa na klabu hiyo.

Aidha, uongozi wa Yanga umeomba radhi kwa wanachama, mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu kwa usumbufu wowote uliojitokeza kupitia sintofahamu hiyo.

Send this to a friend