Yanga yaachana na Saido

0
46

Uongozi wa Klabu ya Young Africans (Yanga SC) imetoa shukrani zake za dhati kwa mchezaji Said Ntibazonkiza (Saido) ambaye amemaliza mkataba wake leo Mei 30, 2022.

“Yanga SC tunamshukuru sana Ntibazonkiza kwa kipindi chote alichokuwa nasi na tunamtakia kila la kheri na mafanikio katika maisha yake ya soka nje ya klabu ya Yanga SC,” imeeleza taarifa ya klabu.

Mchezaji huyo ambaye ni raia wa Burundi ameitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili tangu alipojiunga na klabu hiyo.

Hivi karibuni Saido pamoja na Dickson Ambundo walisimamishwa na uongozi wa Yanga kwa sababu za kinidhamu.

Uamuzi huo ulifanyika baada ya Saido na Ambundo kuondoka kambini walipokuwa mkoani Shinyanga kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa nusu fainali ya ASFC uliofanyika Mei 28 dhidi ya Simba SC na Yanga kuibuka kinara kwa bao 1 kwa 0.

Send this to a friend