Yanga yaeleza sababu ya kumuuza Fei Toto Azam FC

0
44

Uongozi wa Yanga SC umesema kilichofanyika hadi klabu hiyo kukubali kumuuza mchezaji Feisal Salum ni kitendo cha Azam FC kugonga hodi kiungwana  kwa ajili ya kumnunua mchezaji huyo.

Akizungumza Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe amesema klabu ya Yanga ilitoa machaguzi kadhaa kumhusu mchezaji huyo ikiwemo la klabu yoyote inayomhitaji kufika ofisini kwa ajili ya mazungumzo ya kumnunua.

“Maamuzi ya Yanga kumuuza Feisal Salum ni ‘interest’ ya ‘football’ [maslahi ya mpira wa miguu] asitokee mtu akaingiza dhana nyingine. Interest ya football tuliwaambia toka mwanzo toka maamuzi ya kamati yalivyotoka nini tunataka kitokee kwenye hili jambo, tunashukuru Mungu Azam FC wamekuja front [mbele] wamejitokeza wao na wamesema wako tayari kumnunua, ni jambo la kiungwana”

“Ndio football ilivyo, ukimuhitaji Mtu unaenda kwenye klabu unawambia uko tayari kumnunua Feisal, yamefanyika mazungumzo, dili imekubaliana na klabu tumeshamaliza hiyo biashara” amesema Ali Kamwe.

Aidha, Uongozi umemtaka kila la kheri mchezaji huyo katika kuendeleza kipaji chake.

Send this to a friend