Yanga yafungiwa kwa kushindwa kumlipa aliyekuwa mchezaji wake

0
116

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeifungia Yanga SC kusajili wachezaji mpaka itakapomlipa mchezaji wake, Lazarus Kambole aliyeshinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.

Uamuzi huo ni kufuatia raia huyo wa Zambia kufungua kesi FIFA akidai malipo ya malimbikizo ya mishahara na fidia ya kuvunjiwa mkataba, ambapo Yanga SC ilitakiwa imlipe ndani ya siku 45 tangu kutoka kwa hukumu hiyo, lakini haikutekeleza.

Wakati FIFA ikiifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji wa kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia kufanya uhamisho wa wachezaji wa ndani.

Send this to a friend