Yanga yagoma, yamtaka Fei Toto aripoti kambini haraka

0
50

Klabu ya Yanga imesema imemwandikia barua mchezaji Feisal Salum ya kumtaka aripoti kambini haraka iwezekanavyo na kuendelea kuutumikia mkataba wake kama mchezaji halali wa klabu hiyo.

Taarifa hiyo imekuja baada ya mchezaji huyo kupeleka maombi yake Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Machi 06, 2023 ya kutaka kuvunja mkataba na klabu hiyo.

“Klabu ya Yanga iko tayari kumpokea Feisal Salum na kumjumuisha kwenye kikosi, na kwa kuzingatia sera na utaratibu wa Klabu ya Yanga katika kuwaongezea mikataba wachezaji wake wanaofanya vizuri, uongozi wa Yanga uko tayari kuendelea na mazungumzo na Feisal Salum na wawakilishi wake juu ya kuboresha mkataba wake kama wataridhia,” imesema taarifa hiyo.

Fei Toto apeleka TFF ombi kuvunja mkataba na Yanga

Aidha, klabu hiyo imesema iko tayari kumruhusu mchezaji huyo kuondoka klabuni hapo kwa kuzingatia matakwa ya mkataba na utaratibu wa sheria za uhamisho wa wachezaji zinazotambulika na TFF pamoja na FIFA.

Pia imesema kuwa ikiwa kuna klabu yoyote inahitaji huduma ya mchezaji huyo, Klabu ya Yanga  iko tayari kufanya mazungumzo wakati wowote.

Send this to a friend