Klabu ya Yanga imepeleka malalamiko kwenye Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) juu ya mchezaji wake, Feisal Salum ambaye alitangaza kuondoka kwenye klabu hiyo.
TFF imetoa barua ya wito kwa kiungo huyo kufika katika ofisi ya TFF Januari 04, 2023 ili kujibu tuhuma zilizofunguliwa na uongozi wa klabu ya Yanga.
“Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania imepokea malalamiko dhidi yako kutoka Klabu ya Young African kufuatia mkataba wako na klabu,” imeeleza barua ya TFF kwa Feisal ambaye kwa sasa anadaiwa kuwa nje ya nchi.
Wazee wa Yanga watishia kutonunua bidhaa za Azam kisa Fei Toto
Aidha, Feisal ametakiwa kufika TFF yeye binafsi pamoja na mshauri wake wa kisheria mbele ya kamati ili kujibu malalamiko hayo yaliyotolewa na Yanga.
Desemba 24, 2022 mchezaji Feisal Salum aliandaka barua ya kuwaaga mashabiki wa akidaiwa kuhamia klabu ya Azam, kitendo ambacho hakikukubaliwa na uongozi mzima wa Yanga wakidai ameenda kinyume na mkataba wake unaomalika mwaka 2024.