Yanga yamtaka Fei Toto kuripoti kambini

0
38

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasredine Nabi amemtaka mchezaji wa timu hiyo Feisal Salum ‘Fei Toto’ kuripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ligi kuu na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Nabi amedai baada ya shauri lake kutolewa maamuzi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) angependa kuanza mazoezi akiwa na nyota wake wote akiwemo Fei Toto ambaye ana wiki tatu akiwa nje ya timu hiyo.

“Shauri lake limemalizika na TFF wamesema ni mchezaji halali, hivyo wakati wachezaji wengine wakiripoti kambini Avic Town Kigamboni na yeye anatakiwa kuungana nao kwa ajili ya kupanga mikakati ya ushindi kwenye mechi zinazotukabili ikiwemo kufanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho Afrika,” amesema.

Taarifa ya TCRA kuhusu vocha za simu ‘kupandishwa’ bei

Ameongeza kuwa ameshazungumza na uongozi wa klabu ya Yanga kuhusu wito huo wa kuripoti kambini, na taarifa aliyopewa na uongozi ni kuwa tayari wamempa taarifa ya kuripoti kambini kwa kuwa bado ni mchezaji wao halali.

Kwa upande wa wakili wa mchezaji huyo, Salum Nduruma amedai mteja wake hawezi kuripoti kambini kwa kuwa msimamo wake ni kulihamishia shauri hilo kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Michezo (CAS) ili kupata haki yake.

Ameongeza kuwa mchezaji huyo hakuridhishwa na maamuzi yaliyotolewa na kamati, na kwamba kwa sasa ,Fei Toto, hana mapenzi tena na timu hiyo.

Chanzo: HabariLeo

Send this to a friend