
Uongozi wa Yanga SC umesema mchezo uliopanga kuchezwa leo dhidi ya Simba SC saa 1:15 usiku uko pale pale na hakuna mabadiliko yoyote.
Yanga SC imesema ikiwa kama wenyeji wa mchezo huo, inaamini taratibu zote za mchezo kama inavyoelekeza kwenye kanuni za Ligi Kuu ya NBC ziko sawa na maandalizi yote yako tayari.
Uongozi wa Young Africans SC utapeleka timu Uwanja wa Benjamin Mkapa kama inavyoelekezwa kwenye kanuni, na hatutakuwa tayari kucheza mchezo huu siku nyingine tofauti na leo.
Aidha, klabu hiyo imewaalika uwanjani uwanjani wanachama, mashabiki, wapenzi wa klabu na wadau wengine waliosafiri kutoka mikoani , nchi za Jirani na sehemu mbalimbali duniani kote kuja kushuhudia mchezo huo mkubwa barani Afrika.