Uongozi wa Klabu ya Yanga umesema bado hawafahamu sababu za kutopewa mwaliko katika mkutano wa 44 wa Shirikisho la CAF.
Akizungumza Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga wakili Simon Patrick katika kituo cha redio cha E-fm, amesema walilazimika kufuatilia mkutano huo kupitia mitandao ya kijamii baada ya kukosa mwaliko.
Simon amekiri kuwa klabu ya Yanga ambao ni mabingwa wa nchi walitamani kuwepo katika mkutano huo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soko Duniani (FIFA), Giovanni Vincenzo.
“Bahati mbaya hatujajua kipi kimetokea na sisi (Yanga) kukosa mualiko, tuliamua kutumia fursa ya teknolojia tuweze kufuatilia mkutano huo.” amesema.
Meneja wa Uwanja wa Mkapa aondolewa kwa kushindwa kazi
Aidha Simon ameongeza kuwa, ingawa mkutano huo ni wa CAF lakini ilipaswa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutambua nafasi ya Yanga kushiriki kwenye mkutano huo na kupewa mwaliko.
Chanzo: Mwanaspoti.