Sababu za Yanga kuwasimamisha Saido na Ambundo

0
85

Msemaji wa Young African (Yanga) SC, Haji Manara amethibitisha taarifa za kusimamishwa kwa muda kwa wachezaji wa timu hiyo Dickson Ambundo na Saido Ntibazonkiza kwa sababu za kinidhamu.

Inadaiwa kuwa, wachezaji hao waliondoka kambini na kurejea alfajiri mara baada ya mechi dhidi ya Biashara, kitendo kilichomfadhaisha kocha na pia kwenda kinyume na sheria na matakwa ya kambi.

“Kweli wachezaji hao kocha Nabi ameamua kuwasimamisha kwa wiki hii baadaye akija Dar es Salaam pamoja na uongozi wataona nini kitakachoendelea. Ni kweli Saido na mwenzake mara baada ya mechi yetu dhidi ya Biashara waliondoka kambini na kurejea alfajiri, hivyo kitendo hicho kimemfadhaisha kocha na uongozi wa klabu ya Yanga kwa ujumla, hivyo wameamua kuwasimamisha,” amesema Manara.

Kwasasa Yanga ipo kambini ,mkoani Shinyanga ikijiandaa na mchezo wao wa nusu fainali ya ASFC dhidi ya Simba SC utakaochezwa Mei 28 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.

Send this to a friend