Yanga yazungumzia usajili wa Clatous Chama

0
73

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Young Africa SC, Senzo Mbatha amesema klabu hiyo haiwezi kuzungumzia tetesi zinazoenea mitandaoni kwamba wanataka kumsajili aliyekuwa kiungo wa Simba SC, Clatous Chama.

Kumekuwapo tetesi mitaani kwamba huenda Mzambia huyo akatua jangwani baada ya kutaka kuondoka nchini Morocco alikokwenda mwishoni kwa msimu kujiunga na AS Berkane.

“Yanga inajivunia wachezaji wake waliopo hivi sasa, na mchezaji unayemuongelea ana mkataba na timu yake na tunaiheshimu Berkane ambako mchezaji huyo anacheza. Hatuwezi kuzungumza kwa sasa,” amesema Mbatha akinukuliwa na gazeti la Raia Mwema.

Akiwa Simba katika kipindi cha miaka mitatu, fundi huyo wa mpira alicheza kwa mafanikio makubwa na kuwa kiungo tishio aliyekuwa na uwezo wa kuamua hali ya mchezo.

Kumekuwepo madai kuwa Chama hafurahii mazingira ya Morocco na kwamba anataka kurejea Tanzania, huku tetesi hizo zikienda mbali zaidi na kufafanua kwamba miamba hiyo ya jangwani inataka kunasa saini yake, huku habari nyingine zikieleza kwamba atarejea Simba.

Send this to a friend