Mei 18, kamati maalum iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuishauri serikali kuhusu ugonjwa wa Corona iliwasilisha ripoti yake kwa Rais Ikulu, Dar es Salaam.
Moja na ushauri walioutoa ambao umeibua hisia mbalimbali ni ule wa kuishauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi.
Kutokana na ushauri huo, na kutokana na uliokuwa msimamo wa serikali ya Tanzania ya awamu ya tano kuhusu chanjo hizo, wananchi wamekuwa na mitazamo mbalimbali, baada ya serikali kushauriwa kukubali chanjo hizo;
Hivi karibuni Rais Samia alisema kuwa serikali haitakubali kila itakachoambiwa au kuletewa na kwamba itajiridhisha kwanza na usalama wa chanjo za corona kabla ya kuanza kutumika.