Yasome mashtaka matatu yanayomkabili Mwandishi Erick Kabendera

0
35

Mwandishi wa habari za kiuchunguzi, Erick Kabendera leo Agosti 5 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka matatu yanayomkabili, baada ya kuwa ameshikiliwa kwa siku 7 sasa bila dhamana.

Katika kesi ya kiuchumi namba 73 ya mwaka 2019, Kabendera ambaye awali alikamatwa ikidaiwa kuwa kuna utata katika uhalali wa uraia wake anashtakiwa kwa kuongoza kundi la uhalifu ili kujipatia faida au manufaa mengine.

Katika shtaka la pili mwandishi huyo aliyegonga vichwa vya habari vya vyombo vya kitaifa na kimataifa kutokana kushikiliwa kwake, ameshtakiwa kwa kutokulipa kodi yenye thamani ya TZS 173, 247,047.02 kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika shtaka la tatu, Kabendera ameshtakiwa kuwa utakatishaji wa fedha, ambapo jamhuri imeeleza kuwa alipokea TZS 173,247,047.02 na kwamba alifahamu wakati akipokea kuwa fedha hizo si halali.

Kwa mujibu wa upande wa Jamhuri, makosa hayo yote yamefanyika kwa muda tofauti ndani ya Mkoa na Jiji la Dar es Salaam kati ya Januari 2015 hadi Julai 2019.

Send this to a friend