Yemen: Watu 78 wafariki wakipatiwa msaada wa Ramadhan

0
45

Takriban watu 78 wamefariki katika mkanyagano uliotokea katika mji mkuu wa Yemen, Sana’a wakati wa ugawaji wa chakula cha msaada kwa ajili ya Ramadhan.

Tukio hilo limetokea Jumatano jioni wakati mamia ya watu walipomiminika katika shule moja wilaya ya Bab al-Yemen mjini Sana’a kwa ajili ya kupata msaada wa takribani dola 10 [TZS 23,460] ambazo zilikuwa zikitolewa na wafanyabiashara kwa ajili ya kuadhimisha siku za mwisho za Ramadhani.

Video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha watu wakipiga mayowe huku wengine wakiwa chini wakijaribu kuomba msaada, baadhi yao wakiwa hawatikisiki na wengine wakijaribu kutoa msaada.

Korea kuwalipa milioni 1 kila mwezi vijana wanaosumbuliwa na upweke

Mashahidi wameiambia shirika la habari la Associated Press kwamba watu waliokuwa na silaha walifyatua risasi hewani katika kujaribu kudhibiti umati wa watu na kisha waligonga waya wa umeme ambao ulilipuka na kusababisha hofu miongoni mwa waliokuwa wakisubiri.

Wafanyabiashara mjini humo ambao walipanga tukio hilo la utoaji wa misaada wamekamatwa na uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo, imesema wizara ya mambo ya ndani.

Send this to a friend