Zanzibar: Ashtakiwa kwa kukata viuno hadharani

0
65

Maulid Hussein Abdallah maarufu kama Mauzinde (29) amefikishwa Mahakama ya Mwanzo katika Kijiji cha Mwera Wilaya ya Magharibi Unguja Kisiwani Zanzibar, kwa tuhuma ya kukata viuno hadharani.

Kijana huyo mkazi wa Rahaleo anatuhumiwa kutenda kosa hilo huko Kibole wilaya ya Kati, Kusini Unguja saa 11 jioni, ambapo mshitakiwa akiwa amevalia mtandio alicheza kwa kukata kiuno mbele ya hadhara jambo ambalo ni kosa kisheria.

Mshitakiwa huyo amepinga mashtaka hayo na kuiomba mahakama kumpa dhamana kwa kuwa yupo kituo cha polisi siku nyingi.

Amri ya kupelekwa rumande imetolewa na Hakimu Safia Waziri, baada ya mshitakiwa kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana ambayo yalimtaka kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya TZS 100,000 pamoja na barua zikiambatana na kopi ya kitambulisho cha Mzanzibar.

Mshitakiwa baada ya kushindwa kutekeleza masharti hayo, mahakama ilimuamuriwa kwenda rumande hadi Aprili 25 mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa ushahidi.

Send this to a friend